Home BUSINESS MKURUGENZI MKUU NHC AFANYA ZIARA SABASABA, AELEZA MAFANIKIO YA SHIRIKA

MKURUGENZI MKUU NHC AFANYA ZIARA SABASABA, AELEZA MAFANIKIO YA SHIRIKA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

 Na: Hughes Dugilo, Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),  Bw Hamad Abdallah amesema kuwa Shirika  hilo limeendelea kujiimarisha katika kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora  imekuwa ikishiriki Maonesho haya kila mwaka, kwa kuna kufikia ndoto zao za kumiliki nyumba.

Bw. Abdallah ameyasema hayo Julai 3, 2025, katika ziara yake ya kutembelea Banda la NHC kweye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Sabasaba, yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.

Ameeleza kuwa Shirika hilo limekuwa na desturi nzuri ya kuyatumia Maonesho hayo kila mwaka kukutana nawananchi kuwaeleza jinsi shirika lao linavyotekeleza majukumu yake, nakwamba wameluwa wakipata wateja kila mwaka.

“Leo tayari kuna wateja tumewapata kupitia kwenye maonesho haya, na tunatarajia mpaka kufika mwisho wa maonesho tutakuwa tumepata wateja wengi.

“Lakini si suala la wateja peke yake, bali pia ni kuufahamisha umma wa Watanzania, NHC inafanya nini, kwani mtu mwingine anaweza akadhani tu inapangisha tu majengo, lakini kupangisha, tunajenga na kuuza nyumba” ameeleza. 

Akizungumzia miradi wanayoisimamia na kuitekeleza, Bw. Abdallah amesema kuwa Shirika hilo lina miradi katika maeneo mbalimbali ambayo wanajenga kwaaajili ya kuuza, ukiwemo mradi maarufu wa Samia Housing Scheme, ambao mpaka sasa wameshauza nyumba 560 kwa awamu ya kwanza, na awamu ya pili ya ujenzi wa nyumba hizo tayari umeshaanza katika eneo la Kijichi.

Aidha, mradi huo wenye jumla ya nyumba 5000 utnatekelezwa kkwa asilimia 50 Jijini dar es Salaam, asilia 30 Jijini arusha, na Asilimia 20, katika mikoa mingine ambayo itakuwa na soko na uhitaji wa hizo nyumba,.

NHC – Golden Premier Residences: Dar es salaam

“Mbali ya Nyumba za makazi, tuna majengo ya Biashara,  ikiwemo Morocco Square huu ni katika ile miradi iliyosimama muda mrefu, lakini umeshakamilika kabisa. na shughuli mbalimbali zikiwemo Shopping Mall, Hotel, Maofisi pamoja.na Nyumba za makazi., tayari zinaendelea, 

National Housing Corporation | ️ MAMBO YANAZIDI KUNOGA KAWE 711 – MITHILI YA VILIMA VYA PARAMOUNT! ✨ Dar es Salaam yazidi kung'ara kwa miradi mikubwa ya kisasa! MRADI... | Instagram

“Lakini pia tuna mradi wa 711 ambao upo Kawe wenye nyumba 422 pamoja na eneo la Biashara mita za mraba elfu 10, ambalo juu ya ghorofa kuna viwanja vya michezo,. Mradi huu pia ulikuwa umesimama muda mrefu, tunamshuru Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ametuwezesha na sasa unakwenda vizuri na tumeanza kufanya finishing. Matarajio ni kwamba tutakapofika mwezi wa 4 mwakani mradi utakuwa umekamilika” amesema Bw. Abdallah.

Pia amezungumzia uendelezwaji wa Mradi mkubwa wa Golden Premier Residence GPR), uliokuwa umesimama kwa muda mrefu, na kusema kuwa tayari mkandarasi amerudi kuaanza kazi kuanzia mwezi uliopita, nakwamba mradi huo wa kisasa utakuwa nae neo la Biashara na makazi, na utachua miaka mitatu hadi kukamilika kwake.

Akizungumzia miradi ya ubia, amesema moja ya maeneo wanayotekeleza miradi hio, ni Kariakoo, nakwamba wanatarajia itakapofika mwishoni mwa mwaka huu kutakuwa na miradi takribani 64 ambayo itafanya eneo la Kariakoo liwe na muonekano mpya kwakua na majengo ya kisasa ambayo la chini kabisa litaanzia ghorofa 10.

Pia Shirika linatekeleza miradi ya Biashara katika mikoa mbalimbali kwa kujenga majengo  mawili ya Biashara mkoani Morogoro, ambao mmoja utakamilika baada ya miezi 2. Lakini kuna mradi mkubwa wa Uruguru Plazawenye eneo laBiashara na Makazi, ambapo mauzo yake yanakwenda vizuri matzo yake yanakwenda vizuri.

Miradi Mingine ni Mkwakwani Plaza uliopo Jijini Tanga, ambao nao ukikamilika utakuwa ni mradi mzuri zaidi katika mkoa huo.

National Housing Corporation | Ndoto za biashara kubwa zinaanzia hapa! Mtanda Commercial Complex inachanja mbuga – hatua baada ya hatua, tunaweka msingi wa mafanikio ya... | Instagram

miradi mingine wanayoitekeleza ni Mtanda Commercial Complex uliopo Mkoani Lindi, unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi miwiwli.

Miradi mingine ni Masasi Complex uliopo Masasi. Mradi wa maduka ya Biashara ulipo Kahama, Tabora Commercial Complex uliopo Tabora, Iringa Complex uliopo mkoaji Iringa, Singida, pamoja na mikoa mingine.