Home LOCAL FCC YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA

FCC YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA

Mkurugenzi wa Tafiti, Muungano wa Makampuni na Uraghibishi wa Tume ya Ushindani FCC, Bi. Zaytun Kikula, ametembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara lililojumuisha Taasisi 14 zilizopo chini ya Wizara hiyo, kuona namna wanavyotoa huduma zao kwa wananchi, katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara, Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi Julai 7, 2025, na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Akiwa katika Banda la FCC, Bi. kikula amepongeza maandalizi yaliyofanywa na Tume hiyo, huku akishiriki katika kutoa elimu ya masuala ya ushindani, kwa wananchi mbalimbali waliojitokeza kutembelea Banda hilo.

Akizungumza alipokuwa akitoa elimu kwa wananchi, amesema jamii inapaswa kuelewa haki zao za msingi zinazotumika katika kumlinda mlaji, pamoja na kuzifahamu sheria zilizopo zilizowekwa kwaajili ya kumsaidia mwananchi.

Aidha, ametoa mwito kwa wananchi mbalimbali kuendelea kutembelea katika Banda hilo ili kujifunza na kupata elimu kutoka wa wataalamu walipo katika taasisi hiyo.

Maonesho ya Sabasaba 2025, yameanza rasmi Juni 27, amapo yanatarajiwa kufungwa rasmi Julai 13, Mwaka 2025.