

Na: Hughes Dugilo, Dar es Salaam.
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imeendelea kutoa elimu ya utambuzi wa alama za usalama katika noti, kwenye maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba, yaliyofikia tamati rasmi leo Julai 13 2025 Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa mahojiano maalum kwenye Maonesho hayo, Afisa kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, BoT, Vitus Chaila, amesma elimu na mafunzo hayo, yanalenga kutambua noti halali za kitanzania kwa kutumia njia mbalimbali zilizowekwa ili kumsaidia mwananchi..

Amezitaja Njia hizo kuwa ni pamoja na utambuxi wa kuona kwa macho halisi ya kibinadamu, kugusa na kuhisi, ambapo njia hiyo ni mahususi kwa watu wenye ulemavu wa macho.
Aidha, njia nyingine ni utambuzi wa kutumia mwanga wa zambarau unaosaidia kuakisi alama muhimu katika noti na kutoa utambuzi kama ni halali au bandia.
“Benki Kuu tumekuwa tukitoa elimu tofauti tafaut kwa walemavu kutambua noti halali na isiyo halali, kwa kugusa na kuhisi zile alama muhimu zilizopo kwenye noti”
Kwa upande wake Lissa Mollel- Afisa, kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, BoT, ametoa rai kwa watanzania wanaofanya malipo ya hela nyingi, kutumia njia za Kibenki kufanya malipo hayo, kwaajili ya usalama utakaopelekea kuweza kutambua kwa haraka noti halali na Bandia.
Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikitumia Maonesho mbalimbali yakiwemo ya Sabasaba, kutoa elimu kwa wananchi namna wanavyotekeleza majukumu yao.






