Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la CRDB, Yanga SC, imeibuka Bingwa kwa mara nyingine kwa kuichapa timu ya Singida BS bao 2-0.
Mchezo huo umepigwa leo Juni 29, 2025, katika Dimba la New Amani Complex Zanzibar, ukichezeshwa na mwamuzi Ahmed Arajiga, kutokea Katesh, Manyara.
Magoli ya Yanga yalifungwa na Kiungo Mshambuliaji wake Duke Abuya katika kipindi cha pili cha mchezo huo, lililowapeleka kwenye mapumziko, ambapo goli la pili likipachikwa kambani na Clement Mzize katika kupindi cha pili cha mtanange huo.
Timu ya Yanga imeendelea kuonesha ubabe wake katika soka la Tanzania ikibeba Kombe hilo kwa mara nyingine, ambapo msimu uliopita, ilitwaa ubingwa huo kwa kuichapa timu ya AZAM FC kwa mikwaju ya Penati 6-5, mchezo uliopigwa Juni 2 ,2024 katika Dimba la New Aman Comlex, Zanziba,