Home LOCAL KHERI YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU 1447

KHERI YA MWAKA MPYA WA KIISLAMU 1447

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatoa salamu za heri na baraka kwa Waislamu
wote nchini Tanzania na duniani kote katika kuukaribisha Mwaka Mpya wa
Kiislamu 1447 Muharram.

Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi, amesema mwaka mpya wa Kiislamu ni fursa adhimu ya kutafakari maisha ya Mtume Muhammad S.A.W, hususan ujasiri wake, uvumilivu, na moyo wake wa kujitolea kwa ajil ya kuleta haki, amani na mshikamano wa kijamii.

“Kwa niaba ya CCM na kwa niaba yangu binafsi, nawatakia Waislamu wote mwaka mpya uliojaa mafanikio, afya njema, amani na mshikamano. Tunathamini sana mchango wa jamii ya Waislamu katika kujenga taifa letu, kukuza maadili, kuimarisha uzalendo, na kudumisha umoja w a kitaifa,” amesema Katibu Mkuu.

Aidha, Balozi Dkt Nchimbi ametoa wito kwa Watanzania wote, bila kujali tofauti
za kidini, kuuenzi mwaka huu kwa kudumisha misingi ya mshikamano wa itaifa, kuvumiliana, na kushirikiana katika kulijenga taifa kwa misingi ya haki utu na maendeleo endelevu.

CCM inasisitiza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa nchi ya amani, umoja na maendeleo kwa
wote.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Balozi DKt. Emanuel John Nchimbi
KATIBU MKUU CCM