Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umefanikiwa kuwalipa fidia wafanyakazi na wategemezi wao 19,650 waliopata madhira mbalimbali ikiwemo ajali, kuugua au kufariki kutokana na Kazi.
Hayo yameelezwana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma, akizungumzia mafanikio ya WCF yaliyopatikana ndani ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, kagika kikao kazi na Wahariri wa Vyombo vya habari, kilichofanyika leo Mei 15, Jijini Dar es salaam, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Dkt. Mduma amesema mafanikio mengine ambayo wameyapata ni kuongeza mafao saba makuu ambayo ni pamoja na fao la ulemavu wa kudumu, fao la pensheni kwa wategemezi, fao la wasaidizi wa mgojwa , fao la utengamano na fao la msaada wa mazishi.
Maafanikio mengine ni uboreshaji wa mifumo ya TEHAMA, ambapo kwa hivi sasa, Mfuko huo tayari umetekeleza mapinduzi ya kidigital kwa zaidi ya asilimia 90% ambapo huduma zote zinapatikana kwa njia ya Mtandandao.
“Mfuko umeendelea na kampeni mbalimbali za elimu na uhamsishaji kwa waajiri na wafanyakazi juu ya haki zao, taratibu za fidia na usalama mahali pa kazi. Elimu hii imesaidia kupunguza ajali na magojwa kazini, pamoja na kuongeza usajili wa waajiri,” amessma Dkt. Mduma.
Mbali na mafanikio hayo, Dkt. Mduma pua amesema Juni, mwaka 2024 WCF ilipata cheti cha, ithibati cha ISO (ISO Certification) kwa utoaji wa huduna bora kwa viwango vya Kimataifa, jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kkikubwa kuleta matumaini wadau wao.
Amesema kuwa mwaka 2023 mfuko huo ulipata Tuzo ya ISSA, (International Social Security Association) kwa matumizi bora ya TEHAMA, na mwaka huu 2025, WCF ilishika nafasi ya pili katika Tuzo za eGA, sambamba na kushika nafasi ya tatu kwenye Tuzo za TEHAMA 2025 kwa Taasisi za umma zilizofanikiwa kuondoa urasimu kupitia TEHAMA.
Pamoja na mafanikio hayo, Dkt. Mduma amesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi ikiwemo waajiri kutosajili na kuwasilisha michango kwa wakati.
“Baadhi ya waajiri bado hawajatekeleza matakwa ya sheria ya kuwasajili wafanyakazi na kuwasilisha michango kila mwezi. Hili linawanyima haki wafanyakazi wanapopatwa na majanga kazini,” amesema.
Aidha, Dkt. Mduma lisisitiza kuwa wataendelea kuboresha huduma, kushirikiana na wadau wote, na kuhakikisha wanasimamia kwa ufanisi utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi ili kila mfanyakazi anapopatwa na madhira apate haki yake kwa wakati.