Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 23, 2025 amewasili Osaka nchini Japan kumwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya kimataifa ya Osaka (World Expo 2025 Osaka).
Akiwa nchini Japan, Mheshimiwa Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.
Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yalianza tangu Aprili 13, 2025 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025, hii ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho haya ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).