Home LOCAL TAMISEMI YAANZA KIKAO KAZI KWA MAAFISA HABARI,UHUSIANO NA MAWASILIANO NCHINI

TAMISEMI YAANZA KIKAO KAZI KWA MAAFISA HABARI,UHUSIANO NA MAWASILIANO NCHINI

Ofisi ya Rais-TAMISEMI yaanza kikao kazi kwa maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano nchini

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Maafisa Habari, Uhusiano, Mawasiliano na Masoko kutoka Halmashauri, Mikoa na Taasisi zilizopo chini ya Ofisi ya Rais-Tamisemi wakifuatilia mada mbalimbali katika kikao kazi kilichoandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Kikao hicho, kimeanza leo tarehe 23/05/2025 katika Ukumbi wa Jiji la Dodoma-Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Katika kikao hicho baadhi ya mada zinazotatajiwa kuwasilishwa leo ni mchango wa TARURA katika mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwenye Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara, mchango wa kuhabarisha miradi ya sekta ya Afya ya msingi, umuhimu wa kuhabarisha kuhusu Elimumsingi, jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii, nafasi ya afisa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 na mchango wa Halmashauri katika Serikali ya Awamu ya Sita.

Lengo la mada hizo ni kuwajengea uelewa maafisa habari wa Halmashauri, Mikoa na Taasisi za zilizopo chini ya Ofisi ya Rais- TAMISEMI kutoa taarifa za utekelezaji wa taarifa sahihi za miradi ya Serikali.