WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na sekta binafsi katika kuimarisha ustawi wa jamii nchini.
Amesema hayo leo Ijumaa (Mei 02, 2025) alipomwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika miaka 100 na mkutano wa 100 wa Rotary International District 9214 kanda ya Tanzania na Uganda, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa The Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
“Serikali yetu imedhamiria kuendelea kukuza ushirikiano wa dhati na wana-Rotarian wote ili kwa pamoja tuendelee kukuza ustawi wa Tanzania.”
Amesema kuwa kazi kubwa zinayofanywa na Club ya Rotari zimesaidia kuboresha hali za maisha ya wenye uhitaji kwenye sekta ya afya, maji na elimu.
Amezemq juhudi zao zimeonekana kuanzia uchimbaji wa visima vijijini, uwekaji wa samani na ukarabati wa shele na kuweka vifaa katika vituo vya afya.
Aidha, Waziri Mkuu amesema kuwa hivi karibuni Mheshimiwa Dkt. Samia alitunukiwa tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” kutokana na matokeo makubwa ambayo yamepatikana kwenye uongozi wake ikiwemo kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 80.
“Zaidi ya hayo, katika kipindi cha uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia, Serikali imeongeza kwa kiasi kikubwa ufadhili wa huduma za afya, kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba, na kujenga zaidi ya vituo 530 vya kujifungulia ili kupunguza vifo vya uzazi, vifo vya watoto wachanga na vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano.”
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Daniel Sillo amesema kuwa Wizara hiyo inatambua juhudi kubwa zinazofanywa na Rotari nchini. “Hata hivyo ninawakumbusha umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya usajili yaliyowekwa na msajili wa jumuiya za kijamii”
http://SERIKALI INATHAMINI KAZI INAYOFANYWA NA SEKTA BINAFSI-MAJALIWA