Home LOCAL SEKRETARIETI YA MAADILI YAPIGA HATUA KUBWA MATUMIA YA TEHAMA

SEKRETARIETI YA MAADILI YAPIGA HATUA KUBWA MATUMIA YA TEHAMA

Dar es SALAAM

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

KAMISHNA wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Sivangilwa Mwangesi, amesema katika kutekeleza sera ya Serikali mtandao, ambapo taasisi zote za umma zinatakiwa kutumia mifumo ya TEHAMA, wamejipanga kikamilifu kutekeleza sera hiyo, nakwamba wamepiga hatua kubwa katika uboreshaji wa majukumu yao baada ya kuanza kutumia Teknolojia hiyo.

Jaji Mwangesi ameyasema hayo alipokuwa akifungua kikao kazi kati ya Tume hiyo na Wahariri wa vyombo vya habari nchini, kilichofanyika leo, Mei 30, 2025, Jijini Dar es Salaam.

Akisoma hotuba yake iliyolenga kuelezea Mafanikio ya Tume hiyo, Jaji Mwangesi amesema, kupitia mifumo hiyo wanapokea kwa urahisi matamko kuhusu mali na madeni ya watumishi wa umma, nakwamba hiyo ni hatua kubwa ya maboresho ya utendaji wao wa kazi, ambapo umepelekea kupunguza adha na gharama kwa wadau wao kufika kwenye vituo vya Tume kupata huduma.

“Matumizi ya mfumo huu ni hatua kubwa ya maboresho ya utendaji wetu na kuwajali wadau na kuwapunguzia adha na gharama ya kufika kwenye vituo vyetu,” 

“Mfumo huu umeanzishwa ili kutekeleza sera ya Serikali mtandao, ambapo Serikali imeagiza taasisi zote za umma kutumia mifumo ya TEHAMA kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano na kuboresha utendaji.” amesema Jaji Mwangosi.

Aidha, ameongeza kuwa, kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wadau kuutumia mfumo huo kwa asilimia tisini, na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali.

“Kwa nafasi hii, nawapongeza watumishi wote wa umma kwa kutupa ushirikiano. Pia navishukuru vyombo vya habari kwa kuutangaza mfumo huu,” ameongeza.

Kwa upande wake Katibu Msaidizi Idara ya Ukuzaji Maadili Fabian Pokela, akizungumzia umuhimu wa mfumo huo wa TEHAMA, amesema unasaidia kulinda uadilifu, huku akisisitiza kwamba, wanaendelea kuuboresha ili ufanye kazi kwa ufanisi zaidi.