Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezungumza kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Kimataifa wa kusaidia Mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) Bw. Peter Sands kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Mfuko huo na Tanzania, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Mei, 2025.