Home LOCAL RAIS DANIEL CHAPO AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA KIKAZI

RAIS DANIEL CHAPO AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA KIKAZI

http://RAIS DANIEL CHAPO AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA KIKAZI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Daniel Chapo tayari amewasili Zanzibar akitokea Jijini Dar Es Salaam ambapo akiwa Zanzibar atakua na ziara fupi ya kikazi 

Akiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume amepokelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Hamza Hassan Juma pamoja na viongozi wengine akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Nchini Tanzania Mheshimiwa Mahmoud Thabit Kombo 

Rais Chapo atakutana na Mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi pamoja na kutembelea kituo cha Uvuvi cha Bahari kuu Fumba