Home Uncategorized OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YAWALETA PAMOJA TEF, PPRA KATIKA KIKAOKAZI

OFISI YA MSAJILI WA HAZINA YAWALETA PAMOJA TEF, PPRA KATIKA KIKAOKAZI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF katika kikao hicho Bakari MachumuMkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Sabato Kosuri (kulia), akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Bakari Machumu (kushoto), katika kikaokazi kati ya PPRA na Jukwaa hilo, kilichoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR), kilichofanyika Mei 12, 2025, Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri akifafanua jambo katika kikao kazi hicho. 

Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF katika kikao hicho Bakari Machumu

Dar es Salaam, Mei 12, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Bw. Denice Simba, amesema kuwa mahali popote panapohusisha matumizi ya fedha nyingi, ni lazima kuwe na usimamizi madhubuti ili kuhakikisha uwajibikaji kwa wote wanaotoa huduma au bidhaa katika taasisi za umma.

Simba ameyasema hayo katika kikaokazi kati ya Taasisi hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kilichofanyika Jijini Dar es Salaam,  chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, (TR).

Katika Kikao hicho, Mkurugenzi huyo aliwasilisha mada kwa Wahariri, nakusema kuwa utekelezaji mzuri wa ununuzi wa umma unahitajika na mamlaka madhubuti ya kusimamia watoa huduma pamoja na wanunuzi kutoka taasisi mbalimbali, ili shughuli hizo ziweze kufanyika kwa ufanisi na kuchochea maendeleo ya haraka.

Aidha, amesema kuwa uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Serikali imeamua shughuli zote za ununuzi wa umma zifanyike kwa njia ya kidijitali kutokana na changamoto za mfumo wa kawaida katika manunuzi.

“Lengo kubwa ni kuboresha ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao kwa kuongeza uwazi, kuzuia mianya ya rushwa, kupunguza gharama na muda wa mchakato, pamoja na kuimarisha ushiriki wa wazabuni wa ndani na nje ya nchi”

Kwa mujibu wa Simba, hadi kufikia sasa jumla ya wazabuni 33,470 wamesajiliwa katika mfumo huo. Tangu Aprili mwaka huu, mikataba na malipo yote ya ununuzi wa umma yameanza kufanyika ndani ya mfumo huo wa kidijitali.