Home LOCAL NCT, JKCI WASAINI MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA

NCT, JKCI WASAINI MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA

 

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Dar es salaam 30.04.2025

Chuo Cha Taifa cha Utalii (NCT) wametia saini Hati ya Mashirikiano na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

Akizungumza katika hafla fupi ya makubaliano hayo, iliyofanyika leo April 30,2025, Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii(NCT )Dkt. Florian Mtey, amesema kuwa hatua hiyo ni katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuimarisha sekta ya utalii nchini.

“Makubaliano haya yanakwenda kujengeana uwezo kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo utalii wa matibabu, ikiwemo kufanya utafiti, kuandaa machapisho, fursa za kujifunza kwa vitendo kwa wanafunzi, pamoja na kuwajengea uwezo watumishi.

Ameongeza kuwa sekta ya utalii ni muhimu katika Taifa kwani inachangia asilimia 17 ya pato la Taifa, nakwamba imeleta tija kubwa kwa Taifa.

Sekta hii imeleta tija kubwa katika uchumi wa nchi kwani imeajiri watu takribani milioni 1.4 kwa mwaka mmoja na kuongeza ajira kwa wananchi” amesema Dkt. Mtey.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge, amesema kuwa makubaliano hayo yamekuja wakati sahihi kutokana na kukua kwa utalii wa matibabu, nakwamba kunahitajika watu wenye weledi wa kutosha watakaotoa huduma bora kwa wageni. Ameleza kuwa mafanikio yaliyopatikana kwenye utalii yanatokana na kazi kubwa ya Rais Samia ya kuifungua sekta hiyo.

“Nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano waTanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mengi makubwa ambayo ameyafanya nchini kwetu ikiwemo uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Afya.

“Hapa kwenye Taasisi yetu ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuna uwekezaji mkubwa ambao umefanyika kwenye maeneo mbalimbali yakiwemo vifaa tiba, rasilimali watu na teknolojia, ambao umeifanya Taasisi yetu kuwa Taasisi kubwa ya moyo duniani, lakini kimbilio kwa nchi za Afrika” amesema Dkt. Kisenge.