Home LOCAL MHE- DKT.MWIGULU NCHEMBA AHANI MSIBA WA DAVID CLEOPA MSUYA.

MHE- DKT.MWIGULU NCHEMBA AHANI MSIBA WA DAVID CLEOPA MSUYA.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amefika kuhani msiba wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, na ambaye pia aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (1973–1975) na Waziri wa Fedha na Uchumi (1986–1989), Hayati David Cleopa Msuya, nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na familia ya Hayati Msuya, Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa, Hayati David Cleopa Msuya atakumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa katika uongozi wake wakati wa uhai wake ikiwemo kuweka misingi imara ya usimamizi wa uchumi wa nchi akiwa Waziri wa Fedha na nafasi nyingine alizozishika na kwamba wataenzi mchango wake huo kwa kuhakikisha kuwa uchumi unazidi kuimarika kwa manufaa ya wananchi.