Home LOCAL MFUKO WA UFADHILI WA MRADI WA PURE GROWTH WAFUNGUA MLANGO WA MAOMBI...

MFUKO WA UFADHILI WA MRADI WA PURE GROWTH WAFUNGUA MLANGO WA MAOMBI NA MAPENDEKEZO YA NISHATI SAFI NA BIASHARA ZA KILIMO NCHINI

Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar, Tanzania – 27 Mei 2025. Taasisi inayojihusisha na Ubia wa Nishati Jadidifu na Ufanisi wa Nishati (REEEP) inajivunia kutangaza kwamba Awamu ya kwanza ya kutuma Maombi na Mapendekezo kupitia mradi wa Mfuko wa PURE Growth Fund Tanzania sasa umefunguliwa rasmi. Mradi huu ni mpango wa kuleta mageuzi katika kukuza ‘Matumizi Yenye Tija ya Nishati Mbadala’ ndani ya mifumo ya kilimo cha chakula ya Tanzania na kufungua njia za maendeleo ya uzalishaji mdogo kwa nchini.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Sambamba na vipaumbele vya Tanzania vya kuimarisha na kukuza maendeleo ya ushindani wa mnyororo wa thamani katika sekta ya kilimo, kupanua upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati katika maeneo ya vijijini na kuongeza sehemu ya nishati jadidifu katika mchanganyiko wa uzalishaji hadi asilimia 75 ifikapo mwaka 2030, Mfuko wa PURE Growth Fund Tanzania unalenga kuzikutanisha kilimo na nishati—sekta mbili ambazo, kwa mujibu wa Shirika la Chakula Duniani (FAO), zinaajiri wafanyakazi zaidi ya 70% wanaoishi nchi za Afrika za Kusini mwa Jangwa la Sahara na kuchangia 20-30% ya Pato la Taifa la ndani barani. Nchini Tanzania, kilimo tayari kinachangia 24.3% ya Pato la Taifa na kinachangia 55% ya ajira zote

Dirisha Moja la Ufadhili Kupitia Mradi wa PURE Growth Fund Tanzania

Dirisha la kwanza la ufadhili chini ya Mfuko wa PURE Growth Fund litatoa EUR 2.5 milioni (zaidi ya bilioni 7.6 za Kitanzania) ya mtaji kama motisha, kiwango cha kuanzia EUR 250,000 – 1,000,000 (zaidi ya milioni 760 mpaka bilioni 3 za Kitanzania) kwa kila kampuni, usaidizi wa kiufundi na ushirikishwaji wa sera ili kusaidia ukuaji endelevu wa Kampuni Ndogo na za Kati za nishati safi na biashara za kilimo, kuziwezesha kupanua shughuli zao, kukuza faida na kujenga msingi thabiti wa wateja. Dirisha la ufadhili litafunguliwa hadi tarehe mosi Agosti 2025, huku awamu ya utekelezaji ikitarajiwa kuanza Januari 2026. Mpango huu unafadhiliwa na msaada kutoka Serikali ya Austria na kutekelezwa na taasisi ya REEEP.

‘’Austria inajivunia kuwa mfadhili wa kwanza wa Mfuko wa PURE Growth Fund, mpango wa mageuzi ambao unaonyesha dhamira yetu ya kukuza mabadiliko ya nishati katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara”, amesema Elfriede Anna More, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Mkuu wa Masuala ya Kimataifa ya Hali ya Hewa na Mazingira, Jamhuri ya Austria.

‘’Programu hii itaondoa hatari kwa sekta binafsi na kuziwezesha kusonga mbele zaidi ya kusambaza teknolojia na kuelekea kuinganisha mifumo ya pamoja, hivyo kupelekea soko thabiti na upatikanaji wa teknolojia na huduma zinazotolewa na Mfuko wa PURE Growth Fund pamoja na minyororo endelevu zaidi ya thamani,’’ amesema Merja Laakso, Mkurugenzi wa Mipango, taasisi ya REEEP.

Kwa kuunganisha teknolojia za Mfuko wa PURE Growth Fund katika mnyororo wa thamani wa kilimo na chakula—kuanzia umwagiliaji na kuvuna mpaka usindikaji, uhifadhi na usafirishaji—mfuko huu utaongeza sehemu ya chakula kinachozalishwa nchini, kupunguza upotevu wa chakula na kuimarisha uwezo wa kustahimili misukosuko ya hali ya hewa na kifedha. Itapunguza zaidi ombwe lililopo kati ya kilimo na nishati mbadala kwa kutoa motisha kwa huduma hizo ambazo zitaongeza manufaa ya teknolojia ya mradi huu kwenye minyororo ya thamani ya chakula cha kilimo.

“Uzinduzi wa Mfuko wa PURE Growth Fund unaashiria hatua kubwa mbele katika dhamira yetu ya kuwezesha jamii zetu kwa kuunganisha ufumbuzi wa nishati jadidifu katika kilimo, na hivyo kuongeza vipato na kuboresha maisha nchini kote Tanzania,” amesema Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Tunayofuraha kuzindua Mfuko wa PURE Growth Fund nchini Tanzania kama hatua ya kwanza katika mpango huu ambao utazifikia nchi nyingi,’’ amesema Eva Kelly, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya REEEP. ‘’Kuna uwezekano wa hali ya juu wa nishati mbadala kubadilisha minyororo ya thamani ya chakula cha kilimo katika nchi zote Kusini mwa Dunia’’.

Biashara Ndogo na za Kati za nishati safi zinazokidhi vigezo na wafanyabiashara wa kilimo wanaofanya shughuli zao nchini Tanzania wanaalikwa kutuma maombi ya ufadhili na usaidizi chini ya Mfuko wa PURE Growth Fund. Miongozo ya maombi, ikijumuisha vigezo vya kustahiki, vipaumbele vya ufadhili na maelekezo ya uwasilishaji, yanapatikana kwa kupakua kwenye tovuti ya taasisi ya REEEP ambayo ni www.reeep.org.

Tarehe ya Mwisho Kutuma Maombi: 1 August 2025