Home BUSINESS MBIO ZA MWENGE 2025 ZAZINDUA MRADI WA NHC WA SH. BILIONI 2.7...

MBIO ZA MWENGE 2025 ZAZINDUA MRADI WA NHC WA SH. BILIONI 2.7 MASASI

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mwandishi Wetu, Masasi,  MTWARA 

Kiongozi wa Mwenge Kitaifa, Ussi amelipongeza Shirika la Nyumba laTaifa (NHC), kwa kazi kubwa ya kutekeleza kwa vitendo ndoto za kuboresha huduma za jamii na wafanyabiashara nchini kupitia sekta ya nyumba, kwa kujenga majengo bora ya kisasa yanayochochea kasi ya maendeleo na uchumi wa taifa.

Ametoa pongezi hizo leo Mei 18,2025 mjini Masasi mkoani Mtwara, wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo
 ipya la biashara (Masasi Commercial Complex) linalojengwa na NHC.

Jengo hilo litakapokamilika litakuwa na
thamani ya Shilingi bilioni 2.7, huku shirika hilo likiahidi kukamilisha ujenzi huo Septemba mwaka huu.

“NHC mnafanya kazi kubwa kwenye sekta ya ujenzi mkiisaidia Serikali kutimiza ndoto za kuboresha huduma na biashara kwa jamii” amesema Ussi.

Jengo hilo la kisasa limejengwa Mtaa
wa Madaraka katika Kata ya Jida, wilayani Masasi likiwa na maeneo mbalimbali ya kibiashara ikiwamo benki,
maduka, migahawa na ofisi za kufanyia biashara mbalimbali,

Akizungumza mara baada ya uwekaji jiwe hilo la msingi, Meneja Uhusiano na Habari wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Muungano Saguya, amesema:

‘Hatua NHC kuwekeza kwa kujenga majengo makubwa mjini Masasi na maeneo mengine ya miji yanayokuwa kwa kasi, ili kuruhusu watanzania kuwekeza biashara zao maeneo hayo
hivyo kuchangia ukuaji uchumi wa Taifa.”

Kwa mujibu wa Saguya, hatua hiyo pia
Itasaidia Serikali kuweza kukusanya mapato yake kwa njia ya kodi kutoka kwa wafanyabiashara, hivyo kusaidia kufikia malengo ya kuliletea taifa maendeleo.

‘NHC inaendelea kutekeleza ujenzi wa
majengo bora ya kisasa maeneo mbalimbali ya miji inayokuwa nchini katika kuchochea maendeleo kupitia sekta ya nyumba nchini,” amesema Saquya

Awali, akitoa taarifa kuhusu mradi huo Mshauri Elekezi wa mradi huo, Noel Mihanjo, amesema kupitia mradi anaousimamia kuna faida mbalimbali ikiwamo kutoa ajira za muda kwa wananchi wakati wa ujenzi, kukuza Uchumi kwa wafanyabiashara na kuleta mwonekano mzuri kwa mji wa Masasi.

“Mradi huu, hadi sasa zimeshatumika
Shilingi 1,450,718,1 59.94″ amesema Mihanjo.

.