WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa Mei 27, 2025, alikutana na Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafirishaji na Utalii wa Japan, Mheshimiwa Hiromasa Nakano kwenye Makao Mkuu ya Wizara hiyo Tokyo Japan
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Wawekezaji katika Sekta ya Miundombinu la Japan (JAIDA) Miyamoto Yoichi pamoja na ujumbe wake ambapo walijadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji kwenye sekta za Ardhi, Miundombinu pamoja na Usafirishaji.