Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amempongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kwa mchango wake katika sekta za afya na elimu sambamba na kusaidia wahitaji jijini Mbeya.
“ Dkt. Tulia anafanya kazi kubwa kwenye sekta ya afya na elimu pamoja na kuwajengea nyumba watu wenye uhitaji. Zile nyumba tunazoziona anawakabidhi watu kumbe tayari kuna nyingine zimejengwa Uyole,” amesema Dkt. Biteko.
Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Mei 10, 2025 jijini Mbeya mara baada ya kukimbia mbio fupi za Tulia (Mbeya Tulia Marathon) katika Uwanja wa Sokoine.