Home LOCAL BRELA YAWEKA KAMBI YA KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA BIASHARA KARIAKOO

BRELA YAWEKA KAMBI YA KUTOA HUDUMA YA KLINIKI YA BIASHARA KARIAKOO

Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka kambi ya kutoa huduma ya Kliniki ya Biashara kwa wafanyabiashara wa Kariakoo.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Kliniki hiyo imelenga kuwahudumia wafanyabiashara wa Kariakoo ili kuweza kuwatatulia changamoto mbalimbali za kiusajili pamoja na zile za Kitehama

Mbali na utatuzi wa changamoto hizo, pia imetumia kliniki hiyo kuwasaidia wafanyabiashara wa Kariakoo kurasimisha biashara zao kwa kuwasajili Majina ya Biashara, Kampuni, Alama ya Biashara pamoja na Leseni za Biashara

Pia ukaguzi elimishi utafanyika kwenye maduka ya wafanyabiashara ili kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na Leseni ya Biashara Kundi A hasa kwa wale wanaofanya biashara yenye sura ya Kimataifa