Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wakati alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Getrude Mongela. Mheshimiwa Majaliwa amefanya ziara ya siku moja wilayani humo ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano.