
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Aprili 14,2025, jijini Dar-es-Salaam, Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Utalii, Ephraim Balozi Mafuru amesema kuwa mchakato wa kupiga kura kwa kanda ya Afrika na Bahari ya Hindi ulifunguliwa rasmi tarehe 11 Machi, 2025 na utafikia tamati tarehe 4 Mei, 2025. Nchi yetu imetajwa katika vipengele zaidi ya 15 ikiwemo Nchi inayoongoza kwa Utalii Afrika (Africa’s leading Destination) – Tanzania,Bodi bora ya Utalii Afrika (Africa’s leading Tourist Board) – Bodi ya Utalii Tanzania, Kivutio Bora cha Utalii Barani Afrika (Africa’s leading Tourist Attraction) Ngorongoro, Mlima unaoongoza Afrika – Mlima Kilimanjaro
Pia amesema, Hifadhi Bora ya Taifa Barani Afrika (Africa’s leading National Park): Serengeti. Pia, Hifadhi za Kitulo, Nyerere, Udzungwa, Mahale, Arusha Tarangire na nyingine zimetajwa katika vipengele vingine kulingana na ubora wake, Uwanja Bora wa Ndege Barani Afrika – Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Bandari Bora Barani Afrika – Bandari ya Dar es Salaam, Fukwe Bora Africa: Zanzibar
“Hivyo ni baadhi tu ya vipengele ambayo vivutio vyetu vimetajwa pia kampuni za watoa huduma za usafiri, malazi na waongoza watalii nchini nazo zimetajwa katika makundi ya tuzo hizi”amesema.
Ameendelea kusema kuwa tukio hilo ni Fursa kwa Tanzania kwa sababu ya kuitangaza Tanzania kama kivutio bora cha utalii Duniani, kwa sababu Wageni kutoka zaidi ya nchi 30 wanatarajiwa kushiriki, wakiwemo wawekezaji, wanahabari wa kimataifa, viongozi wa sekta ya utalii na wadau mbalimbali hivyo basi kupitia jukwaa hilo tutapata nafasi ya kuonesha vivutio vyetu vya kipekee ikiwemo Milima, Hifadhi za Wanyamapori na Misitu, Fukwe, vyakula, tamaduni zetu n.k
Pia ametoa wito kwa wadau wote wa Sekta ya Utalii, Mabalozi, watalii, wasanii, vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika zoezi la kupiga kura kwa vivutio vya Tanzania pamoja na kutoa hamasa kwa wengine ndani na nje ya nchi kupiga kura na kutoa huduma bora kwa wageni ikiwepo malazi, usafiri ,pindihafla hiyo itakapoadhimishwa
Na Kuitumia hafla hiyo kama fursa ya mafunzo, uunganishaji wa kibiashara na kuboresha ushindani wa utalii wa Tanzania kimataifa pamoja na Kufuatilia na kushiriki hafla hii moja kwa moja au kupitia mitandao ya kijamii.



