Home LOCAL SALAMU NA UJUMBE WA RAIS DKT,SAMIA SULUHU HASSAN KWENYE SIKUKUU YA PASAKA...

SALAMU NA UJUMBE WA RAIS DKT,SAMIA SULUHU HASSAN KWENYE SIKUKUU YA PASAKA LEO APRIL 20,2025

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Nawatakia nyote kheri ya Sikukuu ya Pasaka ambapo ndugu zetu Wakristo wanaadhimisha kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo.

Siku hii njema ikawe pia ya tafakari kwetu sote juu ya upendo wetu kwa Muumba wetu na wenzetu; juu ya kujitoa kwa bidii na weledi katika utekelezaji wa majukumu yetu popote pale tulipo; juu ya kuendelea kujenga jamii inayoishi katika kweli; na juu ya haki ambazo daima huambatana na wajibu kwetu sote.

Kwa pamoja, tuendelee kuliombea Taifa letu kheri, huku tukiishi na kutenda yale yanayoiwezesha nchi yetu kuendelea kubaki kuwa moja, imara, yenye amani na utulivu.