Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Mhe. Abdallah Ulega (wa pili kushoto) akipotea msaada wa mitungi ya gesi kutoka kwa Meneja Mauzo wa PumaGas, Bw. Erick Meena (katikati), wakati wa shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani. Pamoja naye wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Hadija Nasri Ali, na kulia ni Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Bw. Ismail Ussi Ali. Msaada wa mitungi hiyo ya gesi ni sehemu ya jitihada za Puma Energy Tanzania kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa uhakika na gharama nafuu nchini kote.
IKIWA NI SEHEMU YA KUUNGA JITIHADA ZA SERIKALI KUHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA NCHINI.
Puma Energy Tanzania imeshiriki katika shughuli za za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani, ambazo ziliongozwa na Waziri wizara ya Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Hamisi Ulega, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Hadija Nasri Ali, na Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Bw. Ismail Ussi Ali.
Kampuni iliwakilishwa na Meneja Mauzo Gesi Puma Energy Bw. Erick Meena, ambaye alikabidhi mitungi ya PumaGas kwa Mheshimiwa Ulega kama ni sehemu ya jitihada za Puma Energy Tanzania kuunga juhudi za serikali katika kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa uhakika na gharama nafuu nchini kote.
Hivi karibuni kampuni ya Puma Energy Tanzania ilizundua upatikanaji wa huduma ya PumaGas jijini Dodoma na kuongeza wigo wake kutoka mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Ikiwa ni jitihada za uungaji mkono wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024 2034), uliozinduliwa Mei 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Kimataifa kuhusu Nishati Safi ya Kupikia jijini Paris ulioandaliwa na Shirika la Nishati Duniani (IEA).
Sasa wateja wanaweza kununua mitungi ya gesi katika vituo vyote vya huduma za kujaza mafuta Dodoma, pamoja na mawakala wa uuzaji wa rejareja. Kampuni pia inatarajia kuzindua maduka mawili ya kisasa ya PumaGas ambayo yatatoa huduma za kisasa, yakiwa na huduma mbalimbali ikiwemo kujaza na kubadilisha mitungi ya gesi, kuhakikisha watu hawakwami katika shughuli zao za kila siku.
Kama hiyo haitoshi, kwa kuanza rasmi upatikanaji wa huduma hii mpya jijini Dodoma, wateja watapatiwa ofa mbalimbali pindi wanunuapo mitungi ya gesi ya ujazo tofauti kama vile 6kg, 15kg, na 38kg. Kwa kuongezea, pia kampuni inategemea kuzindua huduma ya uuzaji wa uuzaji wa nishati kwa wingi au ujazo mkubwa kuanzia 200kg mpaka 20,000kg.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Hadija Nasri Ali, akizungumza wakati wa wakati wa uzinduzi wa shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani. Wakifuatilia hotuba hiyo kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge, Kiongozi mkuu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2025, Bw. Ismail Ussi Ali na kushoto ni Meneja Mauzo wa PumaGas, Bw. Erick Meena. Puma Energy Tanzania imekabidhi msaada wa mitungi ya gesi ni sehemu ya jitihada za Puma Energy Tanzania kuunga juhudi za serikali katika kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa uhakika na gharama nafuu nchini kote.
Mmojawapo wa wananchi waliohudhuria shughuli za Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani, akifurahia bidhaa ya PumaGas.