Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), ukiongozwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Jijini Paris, nchini Ufaransa, Bw. Bertrand Walckenaer, ambapo pamoja na mambo mengine ametoa wito kwa wawekezaji kutoka Ufaransa kuwekeza nchini Tanzania katika Sekta ya viwanda vya kuzalisha dawa za binadamu ili kukabiliana na upungufu wa dawa muhimu za binadamu hali inayosababishwa na mabadiliko sera za nchi mbalimbali duniani.