Home LOCAL BALOZI NCHIMBI APOKELEWA KWA SHANGWE, VYAMA VYA UPINZANI VYAMIMINIKA CCM

BALOZI NCHIMBI APOKELEWA KWA SHANGWE, VYAMA VYA UPINZANI VYAMIMINIKA CCM

Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, mkoani Ruvuma imeanza kwa kishindo, huku mamia ya wanachama wa vyama vya upinzani wakihama na kujiunga na CCM.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Katika mkutano wa hadhara uliofanyika Jumatano, 2 Aprili 2025, katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mlingo, mjini Tunduru, wanachama wa vyama mbalimbali vya upinzani walimkabidhi Balozi Nchimbi kadi zao, wakitangaza kuunga mkono CCM na uongozi wa Mwenyekiti wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi wa ACT Wazalendo wakiongozwa na Katibu wa chama hicho wilayani Tunduru, Ndugu Said Ramadhan Mponda, walieleza kuwa hatua yao ya kurejea CCM imetokana na kuridhishwa na utendaji wa Mhe. Dkt. Samia na uteuzi wa Balozi Nchimbi kuwa mgombea mwenza wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

Miongoni mwa waliorejea CCM ni Diwani wa ACT Wazalendo wa Kata ya Mchoteka, Ndugu Seif Hassan Dauda, na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Kata ya Nakayaya, Bi. Mwajuma Said Ajida. Wakihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza, walikiri kuvutiwa na jitihada za Mhe. Dkt. Samia katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Balozi Nchimbi, ambaye ni mzaliwa wa Ruvuma, yuko katika ziara ya siku tano inayojumuisha wilaya za Tunduru, Namtumbo, Songea, Mbinga na Nyasa, akikamilisha maeneo ambayo hakuyafikia kwenye ziara yake ya mwaka jana.