


Amesema Serikali kwa kutambua hilo imedhamiria kuendelea kushirikiana na wadau wote ili kuhakikisha sekta ya kifedha inazidi kuwa jumuishi, fanisi, na yenye tija kwa maendeleo ya Taifa.
Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!Amesema hayo leo (Jumatatu, Machi 3, 2035) alipozindua huduma mpya za kidijitali za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) katika ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam.
Ameongeza kuwa katika vipindi tofauti, Serikali imekuwa ikiandaa na kutekeleza mikakati ya Taifa ya kuboresha huduma jumuishi za kifedha.
“Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023 – 2028 ni mwendelezo wa mafanikio yaliyopatikana kupitia Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha uliokamilika Desemba 2022”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa jitihada nyingine ni kuandaa Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali wa miaka 10 kuanzia mwaka 2024 hadi 2034. “Mkakati huu umeainisha malengo mahsusi ambayo kama nchi tunaazimia kuyatekeleza ili kufikia uchumi wa kidijitali.”
Kwa upande wake, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Sauda Msemo amesema sekta ya fedha imeendelea kuwa na ustahimilivu na hivyo kuwezesha shughuli mbalimbali za kiuchumi kufanyika.
Aidha, Naibu Gavana huyo ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zifuate viwango bora vya usalama wa mitandao na kugundua haraka pale panapotokea udanganyifu wa aina yoyote.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi alisema lengo la uzinduzi wa huduma hizo za NBC kidijitali ni kuboresha utoaji wa huduma za kifedha na kuzifanya zipatikane kwa urahisi. “Huduma hizo ni pamoja na ufunguaji wa akaunti, kuhamisha fedha, kupata mikopo bila ya kwenda katika tawi.”
Pia, Kiongozi huyo alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kuhakikisha wananchi wengi wana namba za NIDA ambazo zinarahisisha ufanyaji wa biashara, utambuzi wa mtu na hivyo kumuwezesha kufungua akaunti.”Namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mazingira ya kiabiashara nchini.”