Home LOCAL WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MITAMBO YA KUZALISHA OXYGEN KWA MATUMIZI...

WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI MITAMBO YA KUZALISHA OXYGEN KWA MATUMIZI YA HOSPITALI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, kwenye kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

….

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za kudhibiti viwango nchini zihakikishe uzalishaji wa bidhaa  zote zinazozalishwa zikiwemo za afya zinakidhi ubora unaotakiwa na kuweza kushindana katika masoko ya kimataifa.

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 20, 2025) baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mitambo ya kuzalisha oksijeni kwa matumizi ya hospitali, ambapo amesisitiza kuwa soko linatakiwa liwe na bidhaa salama, bora, na zinazokubalika kimataifa. Mitambo hiyo inajengwa katika ofisi za TOL Gases, Temeke Dar es Salaam.

Amesema mradi huo utakapokamilika utazalisha lita milioni 4.1 za oksijeni ya matibabu kwa mwaka kuanzia mwaka 2026. “Hatua hii itaboresha upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na vituo vya afya, pamoja na kupunguza gharama za oksijeni ya matibabu kwa asilimia 35 katika hospitali na vituo vya afya kote nchini, hivyo kuimarisha huduma za afya kwa wananchi”.

Aidha, Waziri Mkuu amesema mradi huu unaunga mkono juhudi endelevu za Serikali za kuhakikisha oksijeni kwa ajili ya matibabu inapatikana kwa urahisi katika kila kituo cha huduma za afya nchini. 

“Mradi huu utaongeza upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na zahanati nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya kupumua ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya akina mama na kuokoa ya watoto wa Taifa hili.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godfrey Mollel amesema mradi huo ni muhimu kwa sababu oksijeni inayozalishwa kwa njia hiyo inakuwa na viwango vikubwa vya ubora , hivyo itasaidia kuimarisha huduma za afya zitolewazo nchini pamoja na kupunguza vifo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases, Daniel Warungu ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujidhatiti katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.

Amesema kampuni yao ya TOL inajivunia kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ya kuboresha huduma za afya, hususani upatikanaji na usambazaji wa gesi ya oksijeni kwa ajili ya matibabu ukiwemo mradi wa shilingi bilioni 9.8 wa ufungaji wa mifumo ya usambazaji gesi wodini katika vituo 129 vya huduma za afya nchini kote.

(mwisho)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara Tanzania Oxygen Limited (TOL), Injinia Daudi Mlwale (kulia), wakati alipoweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, kwenye kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Molel na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Oxygen Limited (TOL), Daniel Warungu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali kabla ya kuizindua, kwenye kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Machi 20, 2025. Temeke jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Oxygen Limited (TOL), Daniel Warungu, wakati akiangalia mitungi ya gesi kwenye gari, baada ya kuweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, katika kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Molel na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara Tanzania Oxygen Limited (TOL), Injinia Daudi Mlwale. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifafanuliwa kuhusu matumizi ya oxygen hospitalen na Mkuu wa Idara ya Fizikia Hospitali ya Rufaa Mkoa Temeke Dokta Ntoli Abraham (kushoto), baada ya kuweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, kwenye kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Molel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mti baada ya kuweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, kwenye kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, kwenye kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea Tuzo ya Umahiri na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Oxygen Limited (TOL), Daniel Warungu, baada ya kuweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, katika kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Molel. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimianana Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Oxygen Limited (TOL), Daniel Warungu, baada ya kuweka jiwe la msingi mitambo ya kuzalisha oxygen kwa matumizi ya hospitali, katika kampuni ya Tanzania Oxygen Limited (TOL), Temeke jijini Dar es Salaam Machi 20, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)