Home LOCAL WASIRA : CCM KWA NAFASI YA URAIS TUMESHINDA MTIHANI

WASIRA : CCM KWA NAFASI YA URAIS TUMESHINDA MTIHANI

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe Dkt. Benson Bagonza wakizungumza nyumbani kwa Askofu wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera.


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, akihutubia Viongozi na wanachama wa CCM Wilayani Ngara akiwa katika mwendelezo wa ziara ya kukagua Uhai wa chama na Utekelezaji wa Ilani Mkoa wa Kamera

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, akipokea kikapu kama ishara ya mavuno mavuno mazuri ya Chakula ya wakulima wa wilaya ya Ngara mkoa wa Kagera, kikapu hicho kimekabidhiwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Ndaisaba Ruhoro.

Na Mwandishi Wetu, Ngara  
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema Chama kimeshinda mtihani kwa kumpitisha Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgombea urais wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu kwa kuwa kulikuwa na watu wengine waliokuwa wanautaka na nyuma yao kuna matajiri wamejicha.
 
Akizungumza na wanachama na wananchi wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, jana, Wasira alitumia nafasi hiyo kuelezea hatua kwa hatua sababu ambazo zimesababisha Chama kumpitisha Rais Samia kuwa mpeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu na miongoni mwa sababu hizo ni utekelezaji mzuri wa Ilani yake ya Uchaguzi Mkuu ya 2020-2025.
 
“Mkutano mkuu uliofanyika Dodoma Januari 18 hadi 19, ukasema kwa mafanikio haya na kwa kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi na Chama Cha Mapinduzi kina wajibu wa kumuweka mgombea, tumemuweka Dk. Samia Suluhu Hassan apeperushe bendera ya CCM kwa nafasi ya urais.
 
“Ukiweka mgombea sheria inataka tuweke mgombea mwenza kwa hiyo tukamteua Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza na baada ya uchaguzi mkuu tutashinda kwa hakika hakuna ubishi katika hili na Samia atakuwa Rais na Nchimbi atakuwa Makamu wa Rais.”
 
Akieleza zaidi Wasira alisema kuwa CCM kupitia mkutano mkuu maalumu wameshampata Dk. Samia Suluhu Hassan na kwamba katika nafasi ya urais kulikuwa na watu wenye uchu na urais
 
“Walikuwepo na wahongaji wanatuambia njooni kwa nini mnamtaka Samia nyie, maana nao watu wenye uchu wa urais wamo wengine wamejificha ficha lakini wamo na wengine wana matajiri nyuma yao wangewapa pesa wajumbe kuwaambia wamkatae Dk. Samia.
 
“Lakini mkutano mkuu maalumu tumeshinda mtihani na nyie wajumbe mnaopiga kura kwa madiwani na wabunge mshinde mtihani wenu kwa kuleta wagombea wazuri wanaokubalika kama anavyokubalika Dk. Samia.
 
Wasira aliyeeleza hayo kwa kirefu alipokuwa anazungumzia ukiukwaji na uvunjifu wa maadili kuelekea uchaguzi mkuu ujao ambao utafanyika Oktoba mwaka huu ambapo alisema Chama kinafuatilia kwa karibu kubaini wanaojihusisha na rushwa kupata udiwani au ubunge.
 
Akifafanua zaidi alisema CCM huko nyuma waliokuwa wanapiga kura ni wachache lakni yamefanyika mabadiliko kwa kuongeza idadi ya wajumbe wanaopiga kura na kuongeza maana sasa hivi mabalozi wote wanapiga kura , kwenye kamati zao za watu wanne kote huko wanapiga kura , kamati za jumuiya zote zinapiga kura , kamati zao za utekelezaji zote zinapiga kura, na watu wengine wengi.
 
“Tunachotaka mjue sababu za mabadiliko hayo, kwanza tunatanua demokrasia ndani ya chama chetu lakini tunataka watu wengi wanaopiga kura wawambie kwa maoni ya wananchi mtusaidie kusema katika watu watatu mmoja katika hawa anamzidi mwengie ili tupate mtu wa kupeperusha bendera ya ccm kati ya hawa watatu.
 
“Tujue wananchi wanasemaje, lakini mimi ni makamu mwenyekiti na kazi yangu moja ni kusimamia maadili hasa watu wanaotaka ubunge ambao baadhi yao wameanza kunyemelea kwa kuvunja maadili.Tunataka mpige kura mkiwa watu huru muimbie CCM mkimsimamisha huyu tutashinda bila tabu kama atakavyoshinda akiwepo Samia,” alisema.
 
Aliongeza kuwa wanaotaka ubunge Ngara na maeneo mengine anazo habari zao wameanza kuvuruga madili wanataka wapigiwe kura kwa fedha wanazowapa wajumbe lakini Bilbia inasema rushwa inapofusha maana yake ni kwamba ukiona mtu anasambaza hela lazima ujiulize kwani hiyo imekuwa huduma?
 
“Kama una hela za kutosha kanunue mahindi kwa bei nzuri ili wananchi wako wafaidike , unasambaza hela unanunua nini? Na hili nalisema kwa wagombea wapya , wabunge waliopo tunachunguza na tunajua mwenendo huo, wanazidisha rushwa mpaka inatia kinyaa sasa nawaambia achaneni na hayo.
 
 “Wacheni kupofusha wajumbe na ninyi wajumbe na mabalozi wa nyuma 10 mtupe heshima ya kutuletea watu wazuri, ndio wajibu wenu maana sisi tumeshampata Samia Suluhu Hassan , wasifikiri kama na kule hakukua na wahongaji wapo tena wakubwa lakni tumeshinda mtihani na ninyi shindeni wenu,” amesisitiza Wasira.
 
Akizungumzia uchaguzi mkuu mwaka huu ,Wasira amewataka wananchi wakiwemo wa Wilaya ya Ngara kujiandaa na uchaguzi huo na kwamba hakuna mwenye uwezo wa kuzuia uchaguzi usifanyike maana amewasikia CHADEMA wakiendelea na kauli yao ya No Reforms No Election lakini ukweli hakuna wa kuzuia uchaguzi mkuu.
 
KUHUSU WAPINZANI
 
Akizungumza kuhusi upinzani alisema wako watu wanauliza kwa nini CCM bado inaendelea kutawal kwa kuwa hawajui historia.
 
“Siku moja nilikuwa na balozi mmoja akaniuliza CCM mnashindaje uchaguzi asilimia 99, nikamwambia huko vijijini hakuna upinzani.
 
“Ndio maana walikosa wajumbe hata wa kusimamisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa, sasa tuwasaidieje nikamuuliza.
 
“Asilimia 60 ya wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa walikuwa wa CCM, vyama vya upinzani havina watu na ushahidi upo mpaka kwenye vijiji vya ngara hapa hawapo,”alieleza.