
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam mapema leo, Machi 24, 2025, Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amesema kuwa ibada hiyo itakuwa ni ya Maandalizi ya kuelekea Uchaguzi.
“Lengo ni kuweka umoja na ushirikiano na watanzania kuombea uchaguzi ili ufanyike kwa amani na kupata viongozi ambao watatuongoza kwa hekima na busara.
“Waimbaji kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Rwanda wanatarajia kupamba tamasha hilo la uimbaji na Maombi ya uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha amewaomba viongozi wa vyama vya siasa kutotumia lugha za matusi katika mikutano badala yake kutumia lugha za siasa zenye heshima na staha.
Pia amewaomba wadau na watu mbalimbali kujitokeza kutoa ushirikiano wa kudhamini tamasha hilo ili kufikia malengo.