Katika Kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani, Maybelline New York bidhaa inayoongoza duniani katika vipodozi imefanya uzinduzi rasmi nchini Tanzania ikimarisha dhamira ya kuwawezesha wanawake kupitia nguvu ya vipodozi.
Halfa ya uzinduzi huo imefanyika Mlimani city Jijini Dar es salaam ikenda sambamba na kusherekea siku ya kimataifa ya Wanawake ambapo Wateja wa Tanzania walipata fursa ya kujifunza na kujionea bidhaa mbalimbali za Maybelline.
Bidhaa hizo ni pamoja na foundations zinazofaa kwa rangi zote za ngozi, rangi nzuri za midomo, na mascara maarufu za bidhaa hiyo ambapo wameleta urembo wa kiwango cha juu kwa bei nafuu.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa Maybelline New York , Victoria Karanja, amesema Bidhaa ya Maybelline zipatikana kwa bei nafuu katika Maduka ya SH Amon pamoja na Maybelline kiosk lililopo Mlimani City Mall kws kuhakikisha wapenzi wa urembo wanaweza kufikia bidhaa kwa uraisi.
“Maybelline New York ni zaidi ya vipodozi, ni kuhusu kujiamini, ubunifu, na kujieleza, Kuingia kwetu katika soko la Tanzania ni hatua muhimu katika kuhakikisha bidhaa za urembo za ubora wa hali ya juu zinapatikana kwa watu wengi zaidi, tukiwahamasisha wakubali uzuri wao wa kipekee,” amesema Killingo.
Ameongeza kuwa upanuzi wa upatikanji wa bidhaa hiyo Tanzanzania unamaanisha kuwa wateja sasa wataweza kufurahia bidhaa za urembo zilizoandaliwa mahususi kukidhi mahitaji yao ya kipekeen na kuathamini upekee wa kila mtu na kuleta mageuzi katika viwango vya urembo.