Home INTERNATIONAL MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Balozi Mhe. Suzan Kaganda anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zimbabwe pamoja na Balozi Mhe. Dkt. Habib Kambanga anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Rwanda. Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Machi 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe. Suzan Kaganda anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zimbabwe mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe tarehe 28 Machi 2025.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe. Dkt. Habib Kambanga anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Rwanda mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe tarehe 28 Machi 2025.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mhe. Suzan Kaganda anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zimbabwe (kushoto) pamoja na Balozi Mhe. Dkt. Habib Kambanga anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Rwanda (kulia) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe tarehe 28 Machi 2025.

……………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi Mhe. Suzan Kaganda anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Zimbabwe pamoja na Balozi Mhe. Dkt. Habib Kambanga anayekwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Rwanda. Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Machi 2025.

Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa na imani waliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuliwakilisha Taifa kwenye nchi hizo. Aidha amewasihi kulinda na kutetea maslahi ya Taifa.

Makamu wa Rais amewasisitiza Mabalozi hao kuwa na takwimu za msingi kuhusu maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania ili kuwa na uwakilishi mzuri katika maeneo yao hususani katika kutekeleza diplomasia ya uchumi. Pia amewataka kufanya jitihada za makusudi kuzifahamu vema nchi wanazokwenda kuiwakilisha Tanzania ili kuweza kujifunza misingi ya ukuzaji wa uchumi wao na kuhamisha maarifa hayo kwa Taifa la Tanzania.

Amesema ni muhimu kwa Mabalozi hao kuweka kipaumbele katika kutafuta maeneo mapya ya ushirikiano ili kuibua fursa zaidi za kiuchumi zitakazosaidia utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi, mbali ya maeneo ya ushirikiano yaliyopo. Amewasihi kujifunza na kuasili mbinu na ujuzi utakaoliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amewasihi Mabalozi hao kueleza maendeleo ya Tanzania katika nchi wanazokwenda kuwakilisha ikiwemo uboreshaji wa Bandari na Miundombinu mbalimbali ya usafirishaji. Pia amesema ni muhimu kuendelea kuitangaza lugha ya Kiswahili katika nchi hizo ikiwemo kutafuta fursa ya ajira kwa walimu wa kufundisha lugha hiyo katika nchi wanazokwenda kuiwakilisha. 

Vilevile, Makamu wa Rais amewasihi Mabalozi hao, kufanya jitihada za kukuza biashara baina ya Tanzania na nchi wanazoenda kuwakilisha kupitia Ukanda Huru wa Biashara Afrika ikiwemo kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa mbalimbali za Tanzania na kuwaunganisha wazalishaji wa Tanzania na  masoko hayo. Pia amewahimiza kukuza ushirikiano na kutekeleza makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano baina ya Tanzania mataifa hayo.

Aidha amewaasa Mabalozi hao kutambua vipaumbele vya Taifa ikiwa ni pamoja na kufahamu takwimu za msingi kupitia rasimu ya Dira ya Taifa, Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Mipango ya Maendeleo ya Taifa. Amesema ni muhimu pia kupata maelezo kutoka kwa watangulizi wao ili kuwepo kwa mwendelezo katika utekelezaji wa majukumu. 

Makamu wa Rais amesema Mabalozi wanapaswa, kuwatambua na kuwaunganisha watanzania wanaoishi katika nchi wanazokwenda kuwakilisha ili kuwa na mawazo ya pamoja na kuwahamasisha waweze kuchangia maendeleo ya Tanzania.