![](https://greenwavesmedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/30-nbcpremierleague-KMC-FC-0-2-Young-Africans-SCtimuyawananchidaimambelenyumamwiko.jpg)
KLABU ya Wananchi Yanga SC, imeiadhibu vikali Klabu ya vijana wa Kino Boys KMC , magoli 6-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Soka ya NBC Tanzania Bara, uliopigwa Februari 14, katika Dimba la KMC Complex, Jijini Dar es Salaam.
Magoli ya Yanga yamefungwa na Kiungo mshambuliaji Aziz Ki akitupia mabao matatu dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti, dakika ya 49 na dakika ya 56 kwa penalti.
Magoli mengine yamefungwa na Prince Dube na Israel Mwenda akikandamiza msumari wa sita katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
Katika mchezo huo KMC walifanikiwa kupata goli moja la kufutia machozi katika dakika ya 51 likifungwa na Redemtus Mussa.
Kufuatia mchezo huo, Yanga inafikisha alama 49 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi ikiishusha Simba wenye nafasi ya pili na alama 47 kibindoni baada ya kucheza mechi 18, huku Yanga wakiwa imecheza michezo 19.
![](https://greenwavesmedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/@pacom_zouzoua-na-mali-70-nbcpremierleague-KMC-FC-1-4-Young-Africans-SCtimuyawananchidaimambelenyumamwiko.jpg)
Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!