Timu ya wenyeji Pamba Jiji FC imekubali kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Yanga SC mbunge iliyopigwa katika Dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mabao ya Yanga yamepachikwa na Shadrack Isaka Boka akifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 28 kwa mpira wa adhabu, huku Aziz Ki akipachika mabao mawili ndani ya dakika moja 75 na 76 na kuifikisha jumla ya mabao 7 katika msimamo wa Ligi.
Kufuatia mchezo huo, Yanga inakuwa imefunga jumla ya mabao 58 kwenye ligi wakiwa vinara na pointi 58. Kwenye mchezo wa leo Yanga walipiga kona 7 ambapo katika hizo sita zilipigwa na Maxi Nzengeli na moja ni Aziz Ki huku Pamba Jiji wao wakipiga kona sita.