Home BUSINESS WATAALAM KUTOKA CUBA WATEMBELEA KRETA YA NGORONGORO KUTAFUTA SULUHU YA MIMEA VAMIZI

WATAALAM KUTOKA CUBA WATEMBELEA KRETA YA NGORONGORO KUTAFUTA SULUHU YA MIMEA VAMIZI

Na Philomena Mbirika, Ngorongoro

Ujumbe wa wataalam kutoka jamhuri ya Cuba wakiambatana watalaam wa uhifadhi kutoka Wizara ya Maliasilii na Utalii wametembelea bonde la kreta lililopo Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuona hali halisi ya uwepo wa mimea vamizi ndani ya Bonde hilo. 

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Akizunguza wakati wa ziara hiyo iliyofanyika leo Februari 18, 2025 Dr. John Bukombe Kutoka taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) amesema lengo la ziara hiyo ni hatua za awali za kutafuta namna ya kukabiliana na changamoto ya mimea vamizi kwenye maeneo yaliyohifadhiwa. 

“Watalaam hawa tutasaidiana kutafuta namna ya kukabiliana na changamoto ya mimea vamizi inayoathiri uoto wa asili ndani ya bonde la Kreta ambayo kwa kiasi kubwa imesababisha kutoweka kwa mimea asili ambayo ni malisho ya wanyamapori” alisema Dr. Bukombe 

Kwa upande wake Kaimu Meneja Kitengo cha Usimamizi wa Wanyamapori na Utafiti, Afisa Uhifadhi Mkuu Lohi Zakaria amesema kuwa NCAA imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kudhibiti mimea vamizi ndani Eneo la Hifadhi ambapo hata hivyo jitihada hizo bado hazijazaa matunda yaliyotarajiwa.

“NCAA tumekuwa tukijitahidi kudhibiti mimea hii kwa kufyeka na kulima njia ambazo hazijaleta mafanikio, tunaamini kwamba ujio wa wataalam hawa ni mwanzo mzuri wa kufikia suluhisho la kudumu” Alisema Lohi.

Dkt. Orlando Enrique Sanchez Leon ambaye ni mkuu wa ujumbe wa wataalam kutoka Cuba alieleza kuwa wameona tatizo la kuwepo kwa mimea vamizi ndani ya bonde la kreta ambapo pamoja na sababu zingine mwingiliano wa shughuli za binadamu na Wanyamapori unaweza kuwa chanzo cha uwepo wa mimea hiyo hifadhi hapo.

Hata hivyo, Dr. Orlando alisisitiza kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wataalam wake kuhakikisha kuwa kutapatikana mbinu bora za kuthibiti mimea hiyo vamizi ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa.