Home LOCAL WASIRA APIGA MARUFUKU UPINZANI KUWATUMIA VIJANA MKOA WA MARA KUFANYA VURUGU MIKOA...

WASIRA APIGA MARUFUKU UPINZANI KUWATUMIA VIJANA MKOA WA MARA KUFANYA VURUGU MIKOA MINGINE

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Stephen Wassira (kushoto)  akizindua Ofisi ya CCM  kata ya Nyakonga iliyopo wilaya ya Tarime, Katika Ziara yake ya kuimarisha chama Mkoani Mara. (Picha na CCM Makao Makuu )
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Stephen Wassira Akizungumza na Wanachama wa  CCM wilaya ya Tarime, Katika Uzinduzi wa Ofisi ya kata ya Nyakonga Katika Ziara yake ya kuimarisha chama Mkoani Mara. (Picha na CCM Makao Makuu )
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Stephen Wassira Akizungumza na Wanachama wa  CCM wilaya ya Serengeti, wakati wa mapokezi  alipowasili Wilayani humo katika muendelezo wa Ziara  ya kuimarisha chama Mkoani Mara. (Picha na CCM Makao Makuu )

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!
Na Mwandishi Wetu 
 
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amesema ni marufuku kwa vyama upinzani kuwatumia vijana kutoka mkoani Mara kama nguvu kazi ya kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali.
Amesema CCM inamipango mizuri kuhakikisha vijana hao wanatumia nguvu zao kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kujikwamua dhidi ya umasikini.
 
Wasira aliyasema hayo jana, alipokuwa akizindua ofisi ya CCM Kata ya Nyakonga wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.
 
‘Nataka niwaambie wananchi wa Tarime CHADEMA wakitaka kufanya fujo mahali popote wanakuja kuchukua vijana Tarime…wanapelekwa kufanya fujo kama majeshi ya kukodi, wakitaka kufanya fujo Mbeya wanakuja, Tarima, wakitaka kufanya fujo sehemu Tarime.
 
“Tunawaambia vijana wa Tarime wana mvua wana jua na Tarima panalimika, kila kitu kinaota tuwasaidie vijana wa Tarime watumie fursa zilizopo…tunawaambia CHADEMA muache kuja kuchukua vijana Tarime, sisi sio eneo la mapambano, vijana wetu sio wa kukodisha kwenda katika mapambano, nasema kama mzee wa Tarime waache kuja kuchukua vijana wa Tarime.
 
Wasira aliwataka vijana wasikubali kuchukuliwa na kutumika katika vurugu kwa kuwa wakienda huko hupigwa, kuumizwa na hata kupata ulemavu kisha kurudishwa Tarime wakiwa na hali mbaya.
 
“Nasema kama mzee wa Tarime, Mzee wa kimila, muache mambo haya mimi najua yanafanyika siku nyingi,” alisema.
 
Kwa mujibu wa Wasira, Tarime ukilinganisha na wilaya nyingine za Mkoa wa Mara ina fursa nyingi zaidi, “hapa tuna madini hapa tuna wachimbaji wadogo na tunataka wachimbaji wadogo walindwe wachimbe kwa amani, tunataka wapewe mafunzo ili wachimbe wapate manufaa kutokana na rasilimali iliyowekwa na mungu katika eneo hili.”
 
Makamu Mwenyekiti Wasira alisema CCM na serikali yake inataka vijana wa Tarime walime kwa kuwa wanayo ardhi wananchi wengi wa wilaya hiyo wa na ujuzi wa kufuga hivyo wanaweza kuifanya Tarime yote kuwa ya ng’ombe wa maziwa.
 
“Kila familia ikawa na ng’ombe wawili wawili ikatufanya tukaweza kujenga kiwanda cha maziwa na watu wa Tarime wakawa wanapata pesa moja kwa moja kila mwezi, hayo ndiyo mambo tunayoyafanya kama Chama,” alisema.
 
AMTAKA WAZIRI WA MALIASILI AFIKE SERENGETI
 
Katika hatua nyingine, Wasira amemtaka Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana kufika wilayani Serengeti kushughulikia suala la mahusiano ya wananchi na Hifadhi ya Serengeti.
 
Alieleza hayo baada ya kupokea kero ya wananchi kuhusu wanyamapori hususan tembo kuvamia makazi na shughuli zao za kilimo.
 
Alisema ni muhimu waziri husika afike Serengeti, ashughulikie tatizo hilo na kutoa ripoti kwa chama kuhusu hatua zilizochukuliwa.
 
“Mahusiano ya watu na Tanapa au Gulmet au Ikorongo, hilo nataka kumuagiza waziri wa Maliasili na Utalii aje ashughulikie mahusiano ya watu hao.
 
“Kwanza suala la wanyama wanaokula mimea ni Tanzania nzima, hilo sio la Mugumu pekee na li akuwa chanzo cha umasikini kwa Watanzania.
 
“Kwa hiyo tunamtaka waziri mwenye dhamana ashughulikie jambo hilo muda mfupi kadiri inavyowezekana na atuarifu ni nini ambacho kinafanywa,” alisema.
 
Wasira anaendelea na ziara yake katika mkoa ya Kanda Ziwa leo akitarajiwa kuingia mkoani Simiyu.