Home SPORTS SIMBA SC YAIZAMISHA NAMUNGO FC 3-0 RUANGWA

SIMBA SC YAIZAMISHA NAMUNGO FC 3-0 RUANGWA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Wazee wa Ubaya Ubwela, timu ya Simba SC, imeirarua vikali timu ya Namungo FC kwa magoli 3-0, katika mchezo wa ligi kuu soka ya NBC Tanzania Bara uliopigwa katika Dimba la Majaliwa Mjini Ruangwa.

Mabao ya Simba yamefungwa na Kiungo Jean Ahoua kwa mikwaju ya penati katika dakika ya 45+8 ya kipindi cha kwanza, na dakika ya 71 ya kipindi cha pili cha mchezo huo, huku Steven Mukwala akishindilia msumali wa tatu katika dakika ya 90 ya mchezo huo.

Katika mchezo huo, mshambuliaji machachari wa Simba Leonel Ateba mwenye magoli 8 katika ligi kuu, ameshindwa kuitumia nafasi ya kuongeza idadi ya magoli, baada ya kukosa mkwaju wa  penati katika dakika ya 51 baada ya kipa wa Namungo kuicheza penati hiyo.

Kufuatia mchezo huo, timu ya Simba SC inasalia katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 50 akicheza michezo 19, huku timu ya Yanga wakiendelea kuongoza Ligi hiyo kwa alama 52 akiwa amecheza michezo 20.