Home SPORTS SIMBA SC KUSHUKA DIMBANI LEO KUIKABILI NAMUNGO FC RUANGWA

SIMBA SC KUSHUKA DIMBANI LEO KUIKABILI NAMUNGO FC RUANGWA

Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC inatarajia kushuka Dimbani kuumana na timu ya Namungo FC ya Ruangwa katika mchezo wa Ligi kuu soka ya NBC Tanzania Bara.

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Mchezo huo utapigwa leo Jumatano Februari 19, katika  Dimba la Majaliwa unatarajiwa kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali nchini kutokana na ushindani mkubwa uliopo katika Ligi hiyo, hasa mbio ya ubingwa kati ya Sumba na watani wao wa jadi Yanga SC.

Simba inashuka Dimbani leo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuondolewa kwenye mbio za ubingwa na timu hiyo mara mbili mfululizo katika uwanja wa Majaliwa.

Afisa Habari wa Simba Ahmed Ally, amewaambia waandishi wa Habari kuwa watacheza kwa tahadhari kubwa kwani wanaiheshimu Namungo hivyo hawataki historia ijirudie.

“Mwaka juzi tulitoaka sare Hapa na Namungo, na baada ya hapo tukapotea kwenye mbio za ubingwa, msimu uliopita pia tulitoka sare hapa kwa bao la kujifunga tukashindwa hata kuambulia nafasi ya pili, sasa tunakwenda kushinda mechi hii muhimu kwani tumeshajua tulipokwamia“ aamesema Ahmed..

Simba SC inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na alama 44, huku watani wao Yanga wakiwa na alama 46 wakiongoza Ligi hiyo. Azam FC wenye alama 39 wanashika nafasi ya tatu, ikifuatiwa na Singida Big Stars wenye alama 34, na Tabora Utd mwenye alama 28 anashika nafasi ya tano.