Home INTERNATIONAL RAIS WA KWANZA WA NAMIBIA SAM NUJOMA AFARIKI DUNIA

RAIS WA KWANZA WA NAMIBIA SAM NUJOMA AFARIKI DUNIA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Rais wa kwanza wa Namibia na mpigania uhuru maarufu, Dk Sam Nujoma, amefariki dunia baada ya kuugua kwa takriban wiki tatu. Taarifa rasmi ya kifo chake imetolewa leo asubuhi na Rais wa Namibia, Dk Nangolo Mbumba, ambaye ameueleza umma wa Namibia kuwa Dk Nujoma alifariki dunia jana usiku saa 5:46 akiwa hospitalini jijini Windhoek.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk Nujoma, ambaye aliongoza harakati za ukombozi wa Namibia dhidi ya utawala wa kikoloni, amekumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuhakikisha nchi hiyo inapata uhuru wake tarehe 21 Machi, 1990. Dk Nujoma alikuwa na uhusiano wa karibu na Watanzania, ambapo alifanya kazi na wapigania uhuru wa nchi hiyo wakati wa harakati hizo.

Kufuatia msiba huu mkubwa, Rais Mbumba ametangaza kipindi cha maombolezo kitaifa, huku serikali ikiratibu taratibu za mazishi ya kitaifa kwa heshima ya kiongozi huyo aliyekuwa shujaa wa Taifa la Namibia.