Home BUSINESS RAIS DKT SAMIA-TUTAIFANYA BANDARI YA TANGA KUWA YA MAALUMU KWA MBOLEA NA...

RAIS DKT SAMIA-TUTAIFANYA BANDARI YA TANGA KUWA YA MAALUMU KWA MBOLEA NA MAZAO YA KILIMO

Na Oscar Assenga, TANGA

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

RAIS Dkt Samia Suluhu amesema kwamba mipango ya Serikali baadae ni kuifanya Bandari ya Tanga kuwa maalumu kwa ajili ya Mbolea na Mazao ya Kilimo nchini.

Aliyasema hayo leo wakati akizungumza na wananchi wa Jiji la Tanga katika Uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni ziara yake ya siku ya sita katika mkoa wa Tanga ambapo alisema wanaamini itachangia pakubwa katika upatikanaji wa ajira kwa vijana.

Alisema kwamba miradi mbalimbali ya BBT ya vijana pamoja na mradi mkubwa wa umwagiliaji wa mkomazi utachangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa ajira na kuongeza fursa kwao.

Alisema kupitia sera za biashara na uwekezaji wanaendelea kurahisisha ufanyaji wa biashara na kuvutia wawekezaji wakubwa mkoani Tanga ambao utaongeza wigo mpana wa ajira kwa vijana.

“Jana tu nilikwenda kuzindua kiwanda cha Chokaa na Saruji cha Maweni Limestone ambacho kimeongeza ukubwa wa kiwanda na ni wazi upanuzi huo unakuja na fursa za vijana ajira zilizofanywa baada ya upanuzi ni 824 na 424 za moja kwa moja na ajira 400 ambazo sio za moja kwa moja sasa viwanda vya aina hiii tutaleta Tanga ili kutoa ajira kwa vijana”Alisema

Alisema kwamba ni kuongeza uzalishaji wa Cocoa, Korosho na Mazao ya Viungo kutokana na kuwa na soko kubwa sana duniani huku akizitaka zile wilaya ambazo zinazalisha mazao hayo waweke jitihada kubwa waingize vijana kwenye mazao hayo kutokana na kuwa na bei kubwa duniani hivyo wanapaswa kuyachangamkia.