Home BUSINESS FCC YAWAJENGEA UWEZO WAHARIRI WA HABARI MABORESHO YA SHERIA KUTHIBITI BIDHAA BANDIA

FCC YAWAJENGEA UWEZO WAHARIRI WA HABARI MABORESHO YA SHERIA KUTHIBITI BIDHAA BANDIA

Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio, Akizungumza katika kikao kazi cha siku moja cha Wahiriri wa vyombo vya habari  kilichofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam.

NA; HUGHES DUGILO, DAR ES SALAAM

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) imekutana  na wahariri wa vyombo  vya habari kwa lengo la kuwajengea uwezo mahususi kuhusiana  maboresho yaliyofanywa kwenye  sheria ya kuthibiti bidhaa bandia  na masuala mengine yanayohusu tume hiyo.

Akizungumza katika kikao kazi cha siku moja cha Wahiriri wa vyombo vya habari  kilichofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio, amesema vyombo vya habari ni mhimili muhimu unaotegemewa kufikisha taarifa kwa umma.

Amesema wanatumia kikao kazi hicho kuwajengea uwezo wahariri hao kuhusu Sheria ya Ushindani iliyofanyiwa marekebisho hivi karibuni ambayo tayari imepitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais.

“Tunalishukuru sana Bunge letu na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kupitisha marekebisho ya Sheria ya Ushindani kwani itarahisisha ufanyaji biashara na uwekezaji nchini,” amesema Erio.

Wahariri hao pia wamejengewa uwezo kuhusu mienendo ya kibiashara inayokatazwa na sheria ya ushindani, tafiti, miungano ya makampuni na uraghbishi pamoja na udhibiti wa bidhaa bandia nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Udhibiti wa Bidhaa Bandia FCC, Khadija Ngasongwa amesema  bidhaa inayoingia sokoni ambayo inafanya kazi zinavyofanya zingine zinaleta ushindani ambao sio halisi

“Kama umechukua nembo ya mtu na ikionekana kwamba ni bidhaa ambayo sio halisi na ukaenda ukashindanisha utakuwa umekiuka utaratubu” amesema

Ameongeza kuwa wizara ya Viwanda na Biashara iliona kwamba sheria  ya kudhibiti bidhaa bandia itakaa vizuri ikisimamiwa na tume ya ushindani fcc.

PICHA NA; HUGHES DUGILO