Home LOCAL DOLA MILIONI 9 KUBORESHA UWEZO WA KITAALUMA CHUO KIKUU HURIA (OUT)

DOLA MILIONI 9 KUBORESHA UWEZO WA KITAALUMA CHUO KIKUU HURIA (OUT)

Na lilian Ekonga
Zaidi ya Dola za Kimarekani milioni tisa zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi inayolenga kuimarisha miundombinu na rasilimali  katika chuo kikuu Huria (OUT) ili kuboresha na kujenga uwezo wa kitaaluma.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa ujenzi wa maabara saba za kisasa za  chuo kikuu huria nchini, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania, Profesa Joseph Kuzilwa, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha fedha hizo zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya sekta ya elimu.
Profesa Kuzilwa amebainisha kuwa uwekezaji huo utasaidia kuinua viwango vya elimu ya juu nchini kwa kutoa mazingira bora ya kujifunza na kufanya tafiti huku 
vikuu huria vina mchango mkubwa katika kutoa elimu kwa watu wengi zaidi, hivyo uimarishaji wa miundombinu utakuwa chachu ya maendeleo ya kitaaluma na kijamii.
Aidha, Profesa Kuzilwa amesema kuwa maabara hizo hazitawanufaisha wanachuo pekee, bali pia watafiti wengine watakaotumia vifaa hivyo vya kisasa kufanya tafiti mbalimbali. 
“Tafiti hizo zitasaidia kuleta suluhisho kwa changamoto zinazokabili jamii na kuchangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali nchini” ameongeza 
Amesema uwekezaji hup utasaidia kuinua viwango vya elimu ya juu kwa kutoa mazingira bora ya kujifunza na kufanya utafiti, hasa kwa vyuo vikuu huria ambavyo vinatoa fursa kwa wanafunzi wengi zaidi kupata elimu bila vikwazo vya kimazingira.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Elias Bisanda, ameweka wazi kuwa miradi ya elimu ya juu haiwezi kuwa na tija endapo fedha zitatumika bila kuleta matokeo chanya katika uchumi wa mwananchi huku akihimiza usimamizi madhubuti wa rasilimali ili kuhakikisha uwekezaji hul unaleta maendeleo endelevu kwa taifa.
Ameongeza kuwa  mradi huo ninaa ujenzi  wa miezi 8 na utajikifa kwenye ujenzi wa maabara katiKa mikoa  saba ya Tanzanaia Bara na inatarajia kukamilika Mwezi june mwakani.
“Maabara  hizi zitakuwa msaada mkubwa kwetu haxa kwa wahitimu wanaosomea kozi za sayansi hapo mwanzo tulikuwa tunakwenda kuomba kwenye vyio vingine. Bisanda
Nae Maratibu wa Mradi wa HEET, Prof. Alex Makulilo amesema mradi huo umegawanyima katika sehem mbili utajikita kwenye ununuzi wa vifaa.