Home BUSINESS DKT. MWAMBA ATETA NA BALOZI WA JAPAN

DKT. MWAMBA ATETA NA BALOZI WA JAPAN

Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!

Na. Josephine Majura WF, Dodoma

Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, kilichofanyika jijini Dodoma, ambapo walijadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii. 

Dkt. Mwamba, aliishukuru Serikali ya Japan kwa kuendelea kuwa wadau muhimu wa maendeleo ya nchi.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Dkt. Johnson Nyella, Kamishna Msaidizi Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckezedeki Mbise, Mchumi kutoka Wizara ya Fedha Bw. Edson Vedasto na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Robert Bendera.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami alipofika Ofisi za Wizara ya Fedha, Dodoma kwa ajili ya mazungumzo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, aliyefika katika  Ofisi za Hazina-Treasury Square, Jijini Dodoma, kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano Kati ya pande hizo mbili.
Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, akizungumza wakati wa kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, baada ya kufika ofisini kwake, Jijini Dodoma, kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Kikao kikiendelea kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, ambaye alifika ofisini kwake kujitambulisha na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami wakiongoza ujumbe wa Tanzania na Japan katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao kati yao, kilichofanyika jijini Dodoma.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba akiteta jambo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Melckzedek Mbise, wakati wa kikao kati yake Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yoichi Mikami, ambaye alifika ofisini kwake Jijini Dodoma, kwa ajili ya kujitambulisha.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano WF, Dodoma)