Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud T. Kombo (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini, Mhe. Nicole Providoli yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam tarehe 18 Februari 2025
Thank you for reading this post, don't forget to subscribe!Madhumuni ya mazungumzo hayo yalikuwa ni Mhe. Providoli kujitambulisha rasmi kwa Mhe. Waziri Kombo baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26 Novemba 2024.
Aidha katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekata ya Afya, maji, TEHAMA, madini na ufadhili wa masomo.
Wamekubaliana pia kuimarisha ushirikiano katika eneo la biashara na uwekezaji kupitia Switzerland – Tanzania Chamber of Commerce (STCC) iliyozinduliwa nchini mwezi Februari 2023.