Kiungo mshambuliaji wa Dar es Saalm Young African’s Aziz Ki amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, dhidi ya KMC, uliopigwa Februari 14, katika Dimba la KMC Complex, Kinondoni Jijini Dar es Salaam
Katika mchezo huo Azizi Ki Stephane alikuwa na wakati mzuri akiifungia timu yake magoli matatu kati ya sita waliyofunga nakuiwezesha timu yake kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 49 wakiwaacha watani wao wa jadi Simba SC kwa alama 1, wenye jumla ya alama 47 wakiwa katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi.
Aziz Ki alionesha kiwango kikubwa cha kusakata kandanda kwenye mchezo huo na kufanikiwa kufunga hat trick yake ya kwanza msimu wa 2024/25 akifikisha mabao matano ndani ya ligi.