Home INTERNATIONAL WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

WAZIRI MKUU AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAPAN

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa  Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe aliofuatana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Januari 14, 2025. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan wa Japan Mheshimiwa Fujii Hisayuki baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, January 14, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa Fujii Hisayuki (kulia kwake) baada ya mazungumzo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi na kulia ni Balozi wa Tanzania chini Japan, Baraka Luvanda. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Yusushi  Misawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
DAR ES SALAAM

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za dini nchini kuendelea kuwahamasisha waumini wake kudumisha amani na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Januari 14, 2025) alipokutana na viongozi wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wapya wa jumuiya hiyo walikwenda kwa ajili ya kijitambulisha.

“Fanyeni kazi kwa uhuru na wala msiwe na mashaka. Wahamasisheni Watanzania washiriki katika shughuli za kimaendeleo.” Pia amewashauri viongozi hao wabuni miradi ya kiuchumi kwani Tanzania kuna fursa nyingi za kimaendeleo.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza jumuiya hiyo kwa uwekezaji iliofanyika katika sekta mbalimbali zikiwemo afya na elimu ambapo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano katika jitihada zao hizo.

Amesema Serikali kwa upande wake inathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi mbalimbali za kidini nchini ikiwemo Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya, hivyo amewahakikishia ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kwa upande wake, Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya, Sheikh, Khawaja Muzaffar Ahmad ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri inayofanywa katika kuwahudumia Watanzania. “Nimeishi Tanzania kwa zaidi ya miaka 20, ni nchi nzuri hongereni kwa kazi nzuri mnazozifanya.”

Naye, Naibu Amiri, Sheikh Abdulrahman Mohammed Ame ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kuwajali wananchi wake na amemuahidi Waziri Mkuu kwamba taasisi yao iko tayari kushirikiana na Serikali katika masuala mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji.

Baadae Mchana, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Bw. Hisayuki Fujii na ujumbe wake kwenye Ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu amemweleza Fujii kuwa Tanzania imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kufanya uwekezaji ambayo yanawawezesha wawekezaji kunufaika na shughuli zao. 

“Serikali inajivunia ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Tanzania na Japan, licha ya yote nchi yetu sasa imeweka mazingira mazuri sana ya uwekezaji Nchini nitumie fursa hii kuwakaribisha kuja kuwekeza Tanzania”

Kwa Upande wake Bw. Hisayuki Fujii, amesema Japan itaendelea kuunga Mkono Ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Japan na kuendelea kuleta wawekezaji zaidi katika sekta ya madini, Nishati na Teknolijia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here