WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa, akizungumza katika Kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika leo Januari 13, 2025 Jijini Dae es Salaam.
DAR ES SALAAM.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa amezindua kampeni ya ‘Perform and Inform’ (tekeleza na taarifu) ya wizara hiyo kwa lengo la kuongeza uwajibikaji na uwazi kwa wananchi.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika kikao kazi kilichoambatana na uzinduzi huo uliofanyika leo Januari 13, 2025 Jijini Dar es Salaam,nakusema kuwa mkakati huo utasaidia wananchi kujua mafanikio ya wizara hiyo na idara zake, lakini pia kuwahisha taarifa kwa wananchi.
“Perform and Inform ni mkakati unaoweza kujuza wananchi mafanikio yaliyopo ndani ya wizara lakini pia kutoa taarifa kwa jamii kwa kuwa, kuchelewesha taarifa kunaweza kusababisha sintoifahamu katika jamii,” amesema Bashungwa.
Akikabidhi kitabu chenye mkakati huo wa mawasiliano kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Waziri Bashungwa amesema mkakati huo wa mawasiliano unahusu wizara yenyewe, Idara ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, pamoja na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Balile amempongeza Bashungwa kwa kujenga utaratibu wa kukutana na wanahabari nakwamba kwa kufanya hivyo, kutaboresha mawasiliano na urahisi wa kupatikana kwa habari.
Balile amemwomba Waziri Bashungwa kuwaeleza wasaidizi wake akiwemo Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), kujenga utaratibu wa kukutana na wanahabari ili kijibu maswali yao na kutolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo.
Aidha, amemweleza Mheshimiwa Waziri kuwa memweleza Waziri Bashungwa kuweka uwanda mpana wa mawasiliano kwa vyama vyote vya siasa hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika baadaye mwaka huu.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodatus Balile, akizungumza kwa niaba ya Wahariri katika Kikao kazi hicho Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA; HUGHES DUGILO