Home LOCAL USAFISHAJI WA VIFURUSHI, MIZIGO NA ABIRIA KIDIJITALI UTAIMARISHA UCHUMI WAZIRI SILAA

USAFISHAJI WA VIFURUSHI, MIZIGO NA ABIRIA KIDIJITALI UTAIMARISHA UCHUMI WAZIRI SILAA

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb), amesema kuwa kupitia mfumo wa usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria Serikali itaimarisha uchumi wa kidijitali, kukuza baishara mtandao na kuleta ajira nyingi kwa vijana hususan madereva wa pikipiki (bodaboda).

Waziri Silaa aliyasema hayo tarehe 24 Januari, 2025 wakati akizundua mfumo wa usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria ujulikanao kama “Swifpack” na kusisitiza kuwa, huduma hii itatoa fursa za kipato cha uhakika, na kuifanya kazi ya bodaboda kuwa sawa na kazi nyingine za usafirishaji wa vifurushi, mizigo, na abiria.

“Leo tunashuhudia hatua nyingine muhimu kwa Shirika la Posta Tanzania kupitia huduma ya Swifpack ambayo itawezesha upatikanaji wa huduma za usafirishaji wa vifurushi, mizigo na abiria kwa kasi, ufanisi na gharama nafuu”, alisema Waziri Silaa na

kuongeza kuwa Teknolojia inabadilisha jinsi tunavyofanya kazi na kuwasiliana, na huu ni mfano bora wa jinsi taasisi za umma zinavyoweza kutumia ubunifu wa teknolojia kutibu mahitaji ya soko na kuboresha huduma kwa wananchi.

Akitoa salamu za Shirika la Posta Tanzania, Postamasta Mkuu Bw. Macrice Mbodo amesema kuwa shirika hilo limeendelea kutekeleza mkakati wake wa nane wa biashara wenye dhamira ya kuifanya Posta ya Tanzania kuwa posta ya Kidijitali kwa biashara endelevu.

“Moja ya mafanikio tuliyoyapata kupitia utekelezaji wa mkakati huu, tumefanikiwa kuunganisha huduma na biashara zetu kwenye programu tumizi inayojulikana kama “posta kiganjani’ inayopatikana playstore na Apple store ambapo kwa sasa kupitia programu hii mwananchi yeyote mwenye simu janja anaweza kufurahia huduma zetu za posta kiganjani mwake ikiwemo kufuatilia mzigo wake (tracking), kuomba na kufanya malipo ya huduma zetu mbalimbali”, alisema Bw. Mbodo.

Aidha, Waziri Silaa alieleza kuwa Serikali ina matarajio makubwa na kwamba huduma hii itachangia kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu kazi za bodaboda, ambazo mara nyingi zimekuwa zikipata sifa mbaya mitandaoni na kutajwa kwa changamoto mbalimbali za kijamii.

Waziri Silaa ameliagiza Shirika la Posta kuhakikisha kuwa linaimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa mizigo na vifurushi (real-time tracking) unafanya kazi kikamilifu, kutoa taarifa sahihi kwa wateja na kuongeza ushirikiano na Sekta Binafsi ili kuhakikisha huduma hii inahudumia wananchi wengi na inafika maeneo mengi zaidi nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here