DAR ES SALAAMThank you for reading this post, don't forget to subscribe!
SOKO la Kariakoo linatarajiwa kufunguliwa rasmi mwezi februari mwaka huu, baada ya kukamilika kwa ukarabati wake kufuatia ajali ya moto iliyotokea Julai 10 202.
Aiidha kufunguliwa kwa soko hilo kutakwenda sambamba na uhakiki wa wafanyabiashara waliokuwa wakifanya shughuli zao ndani ya soko hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 29, 2025 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Soko la Kariakoo, Hawa Ghasia, amesema Uhakiki huo unasimamiwa na timu ya maalum iliyoundwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ikijumuisha wawakilishi wa Wafanyabiashara, Menejimenti ya Shirika la Masoko hilo na vyombo vya Usalama.
“Menejimenti inaratibu kazi ya kutangaza majina ya waliokuwa wafanyabiashara kwenye Soko hilo ambao wamekidhi vigezo na sifa za kurejeshwa baada ya uhakiki” Amesema
Amesema kuwa Uhakiki uliofanywa na wataalamu hao umebaini jumla ya wafanyabiashara1,520 wanaotarajiwa kurejeshwa sokoni nakwamba majina na fomu ya kujiunga vitatangazwa kwa umma kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na tovuti ya OR – TAMISEMI
Pia, amewataka wafanyabiashara wenye madeni kulipa madeni yao kabla ya kurejea sokoni ambapo takwimu zinaonyesha jumla ya wafanyabiashara 366 wanadaiwa na Shirika Shilingi 358,571,106.85.
Soko la Kariakoo lilipata ajali ya moto mnamo tarehe 10 Julai 2021 na kusababisha wafanyabiashara kuondolewa na shughuli kusimama ili kupisha ukarabati.
PICHA NA; EMMANUEL MBATILO