Home SPORTS SIMBA SC YAMALIZA MWENDO, YATINGA ROBO FAINALI SHIRIKISHO

SIMBA SC YAMALIZA MWENDO, YATINGA ROBO FAINALI SHIRIKISHO

Timu ya Simba SC ya Jijini Dar es Salaam Tanzania, imetinga fanikiwa hatua ya robo fainali michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kutoa sare ya bao 1-1 na Fc Bravosya Angola.

FC Bravos ndio walikuwa wa kwanza kuziona nyavu za Simba kwa bao lililofungwa na Abdenego katika dakika ya 13 kipindi cha kwanza cha mchezo huo, huku bao la Simba SC la kusawazisha lilifungwa na Leonel Ateba katika dakika ya 69 ya mchezo huo. 

Kwa matokeo hayo timu ya Simba SC inatinga hatua ya robo fainali ikiwa na alama 10, ikiongozwa na CS Constatine yenye alama 12, huku timu ya Bravos yenye alama 7 wakiungana na CS Sfaxien yenye alama 0 kuaga michuano hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here